Akaunti ya Twitter ya kundi la wanamgambo wa
Al Shabaab imesitishwa kwa mara nyingine.
Ujumbe kutoka kwa Twitter katika akaunti yake ya
@HSMPress1 ulisema kuwa akaunti hiyo
imefungwa, ingawa hapakuwa na maelezo kwa
nini hatua hiyo ilichukuliwa.
Katika taarifa iliyotumwa kwa shirika la habari la
AFP kundi hilo lililaani hatua ya Twitter na
kusema kuwa haitazaa matunda yoyote.
Mnamo siku ya Jumanne, Al Shabaab ilisema
kuwa ilishambulia msafara wa magari ya rais wa
Somalia Hassan Sheikh Mohamud, ambaye
hakujeruhiwa.
Hata hivyo habari hizo zilipuuzwa na ofisi yake
ikisema kuwa rais hakujeruhiwa kwani kifaa
kililipuka mbali sana na msafara wake.
Baadaye kundi hilo lilituma ujumbe kwa Twitter
uliosema kuwa ,''Mara nyingine hautaponea ''kwa
mujibu wa ripoti za , AFP.
Hata hivyo akaunti yake ya kiarabu ingali iko
wazi.
Kwa mujibu wa sera ya Twitter, akaunti
zinazotumika kutuma vitisho,zinapaswa
kufungwa. Akaunti pia zinaweza kufungwa ikiwa
zinatumiwa kwa shughuli zisizo halali.
Taarifa ya Al-Shabab ilisema kuwa haina akaunti
nyingine ya Twitter kwa kiingereza na kuwaonya
watumiaji wa mtandao huo kuwa wajiandae kwa
akaunti zao kuvamiwa.
Akaunti ya Twitter ya kundi hilo kwa jina
@HSMPress, ilisitishwa mwezi Januari baada ya
kundi hilo kuitumia kutuma ujumbe wa kutisha
kuwa lingewaua mateka wa Kenya na kisha
kusema kuwa limefanya hivyo.
Wadadisi wamesema kuwa katika siku za nyuma,
Marekani ililazimisha Twitter kufunga akaunti
hiyo ingawa haikuwa na nguvu za kisheria
kufanya hivyo.
Hata hivyo Twitter inasema kuwa hakuna kitu
kinachoweza kuzuia Al Shabaab kuwa na akunti
nyingine baada ya nyingine za kwanza kufungwa.
Al-Shabab ilifungua akauti yake mara ya kwanza
mwezi Disemba mwaka 2011 baada ya wanajeshi
wa Kenya , kwenda Somalia kupambana na
wanamgambo hao.
Wanamgambo hao wamefurushwa Mogadishu
pamoja na kutoka miji mingine ingawa bado
wanadhibiti sehemu nyingi za Kusini mwa
Somalia.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment